Tuesday, June 26, 2012

MAPISHI LEO - NAMNA YA KUPIKA ROJO YA CARROT

 Kata kata Carrot ziwe nyembamba kwa wingi uupendao/waweza tumia vile vifaa vya kukatia, zote zinakuwa atleast size moja
 Kaanga vitunguu vyako viwe brown
 Weka nyanya ulizoandaa, ziseiwe nyingi sanaa
 Hakikisha zinalainika sana zinakuwa kama uji
 Halafu weka Carrot zako ulizokata kata geuza geuza, uweke na chumvi
 Baada ya hapo weka vitunguu swaumu ulivyotwanga ukachanganya na tangawizi kidogoo. Angalizo tangawizi iwe ni ka kipande kadogo sana, isizidi wingi wa kitunguu swaumu
 Geuza geuza ule mchanganyiko wote kwa pamoja
 Acha uchemke kwa muda, uwe makini isiive sana kama maharage
Halafu ipua Rojo yako, inakuwa tayari kwa kula na ugali,wali,viazi vya kuchemsha,pilau n.k.


Namshukuru Mama Mkwe kunifundisha pishi hili, ni rahisi sana na la haraka, tamu kweli kweli


NB. Hili ni pishi la kibongo bongo hasa nyumbani, angalia wingi wa mboga utakayo ndo ita determine viungo vyako viwe vingi kiasi gani


ENJOY UR MEAL

No comments: