Friday, March 23, 2012

JUISI YA UKWAJU NI SULUHISHO HASA KWA WALE ISIOWADHULU

Nunua ukwaju wako ukiwa wa maganda kama huu, au ambao umeshatolewa maganda

Ukishautoa kwenye maganda, weka kwene bakuli kubwa, chemsha maji yako yawe ya moto halafu mwagia kwenye ukwaju wako, uyaache kwa muda yapoe



Yakishapoa, nawa vizuri mikono yako, anza kupikicha, pikicha sana, ukiridhika kuwa umepikicha vizuri, chuja vizuri kwa chujio safi, hakikisha atleast iwe nzito(conco), isiwe nyepesi sana kama zile tunazouziwa mtaani ni nyepesi sana


Ukishachuja, ihifadhi vizuri, kwenye jagi au popote uonapo itakuwa katika usalama, kama una fridge waweza weka huko, kama hauna usitengeneze nyingi sanaaa zaidi ya glass 4, kuhofia kuharibika

ITUMIKE VIPI HASA KWA WALE WENYE MATATIZO YA KUPATA CHOO
Naomba nielezee jinsi nilivyokuwa natumia mimi na ikanisaidia.
Hakikisha chakula cha jioni unakula isizidi saa 2 usiku, namaanisha ikifika saa 2 usiku uwe umeshapata dinner yako. mfano umekula dinner saa 2 usiku, kaa kwa nusu saa chukua juice yako weka kwenye glass yako, weka sukari ila nashauri utumie ASALI kama unayo ni nzuri kiafya, kunywa glass 2 za juisi ya ukwaju uliyotengeneza mwenyewe,ukihahkikisha umekunywa glass 2( lakini sio unywe kama maji unazinywa kwa pose), tylia kwa nusu saa tena, kunywa glass 2 za maji waweza kunywa kwa interval hadi ukienda kulala uwe umeshakunywa glass 2 za maji.
Ukiamka siku ya pili asubuhi hakikisha umeamka nusu saa kabla ya muda wako wa kuamka siku zote, kama unahitaji matokeo mazuri inabidi uamke, kunywa chai kabla hujapiga mswaki, au maji ya fukuto  glass mbili usinywe ya baridi, baada ya nusu saa waweza pata majibu au la.
Fanya hivvyo kwa wiki nzima, kuna wanaopenda wanywe hiyo juice kila mara, ila kama utakunywa kila mara hakikisha umekula ndio ule, kwani waweza kusikia tumbo likikwangua na kusababisha vidonda, zingatia hilo, ndio maana mimi nilikuwa nakunywa usiku tu, na ilinisaidia sana


KILA LA HERI, MLETE MAJIBU IKIWASAIDIA
MIMI PENDA NYIE SANA, WEEKEND NJEMA

4 comments:

Nuar said...

Hey, Ester!
Thanks a lot for your comment on my blog and for giving me the chance to discover yours, which is very enjoyable!
I'm following you now, and if you like my blog, I'll be thrilled to have you among my followers, as well!
XOXO, María José
http://nuarbarcat.blogspot.com/

Interestedtips said...

ur welcome dear

Anonymous said...

Are still dealing with herbal medicine?

Unknown said...

Thanks